May 23, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga amesema kuwa mashabiki wa Yanga wasiwe na mashaka kuhusu kuondoka kwa Heritier Makambo kwani anashusha mashine kali zaidi yake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kwamba hakuna kinachoharibika ndani ya Yanga kwani tayari amezungumza na wachezaji wengine wazuri zaidi ya Makambo na mazungumzo yamekwenda sawa bila matatizo yoyote.

"Ni kweli Makambo anaondoka Yanga, lakini yeye sio mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa zaidi ya wengine, ninawaleta wengine wakubwa na wanaomzidi Makambo ni jambo la kawaida kwenye maisha ya soka.

"Yeye anaondoka na sisi tunachofanya kumleta Makambo mwingine ambaye atafunga mabao mengi zaidi na wenyewe watamsahau ghafla tu ndivyo ilivyo kwenye soka, kabla ya Juni maana ligi inaisha Mei 28 nitamtaja" amesema Zahera.


1 COMMENTS:

  1. Huyo ikiwa ni kweli na pindi akatokea na uwezo wa Makambo, Zahera haraka atamtafutia mnunuzi na kumpigia bei

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic