June 16, 2019


KWA sasa joto la usajili ndio limepamba moto huku kila timu ikiwa bize kukamiisha usajili wa wachezaji ambao wanawahitaji.

Mpaka sasa tayari mabingwa watetezi Simba wamewatangaza rasmi wachezaji watano ambao wamemalizana nao kila kitu na watawatambulisha rasmi Juni 21 Mwanza.

Hawa hapa ambao wamemalizana na Simba mpaka sasa.

John Bocco, nahodha wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili kwa sasa yupo na timu ya Taifa nchini Misri.

Erasto Nyoni, beki kiraka wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, kwa sasa yupo nchini Misri na timu ya Taifa.

Aishi Manula, Mlinda mlango wa Simba, ameongezewa miaka mitatu, kwa sasa yupo nchini Misri.

Jonas Mkude, Kiungo wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, yupo Tanzania kwa sasa.

Beno Kakolanya, Mlinda mlango wa Simba amesajiliwa akiwa huru, yupo Tanzania.

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic