UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kesho lazima wapambane mbele ya TP Mazembe ili kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kagame.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa hakuna mchezo mwepesi ila wanapeleka timu uwanjani wakitafuta matokeo chanya.
"Tupo vizuri tutakwenda uwanjani kutafuta matokeo chanya, tunashukuru Mungu tupo salama, tumeanza na tunaendelea kuimarika taratibu, timu inaimarika matarajio yetu kufanya vizuri.
Idd Cheche ambaye ni Kocha Msaidizi amesema kuwa wana imani na kikosi chao kwa sasa ambacho kinazidi kuimarika.
Ofisa habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema kuwa Kigali imechangamka na wengi wanauzungumzia mchezo wa kesho.
0 COMMENTS:
Post a Comment