KOCHA Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije ameahidi kutetea ubingwa wa kombe la Kagame ambalo linatarajiwa kuanza Julai 7-21 nchini Rwanda.
Azam FC ni watetezi wa kombe wamepangwa kundi B pamoja na KCCA (Uganda), Mukura (Rwanda) na Bandari (Kenya) wanatarajiwa kukwea pipa kesho kutia timu nchini Rwanda.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wanakwenda wakiwa kifua mbele kupambana kutetea ubingwa kwa mujibu wa kocha Ndayiragije ambaye tayari ameanza kukinoa kikosi hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment