Lionel Messi mshambuliaji wa timu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina amesem kuwa timu yao ya Taifa imeponzwa na maamuzi ya waamuzi kwenye mchezo wa nusu fainali ya Copa America.
Argentina ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Brazil kwenye hatua ya nusu fainali huku Messi ambaye ana tuzo tano za Ballon d'Or uwanja wa Belo Horizonte usiku wa kuamkia leo akiwa hana bahati ya kushinda kombe hilo.
Kumekuwa na mjadala mkubwa kama Messi anaweza kuitumikia timu yake kwenye fainali za kombe la Dunia mwaka 2022 zitakazofanyika nchini Qatar kutokana na nyota huyo kufikisha miaka 35 mwaka huo.
Messi amesema kuwa hawakufanyiwa sawa kwenye mchezo huo kutokana na waamuzi kuwapotezea penalti halali ambazo walizipata kwenye mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment