July 16, 2019

ETTIENE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC, amesema kuwa kwa sasa kwenye michuano ya Kagame Azam FC ndio timu kubwa kuliko nyingine ikiwa ni pamoja na TP Mazembe.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa Azam FC ni kubwa kutokana na kuwa ni mabingwa watetezi hivyo kila timu inayoshiriki inatambua hilo.

"Hapa ukitaka kuzungumzia timu kubwa kwenye michuano ya Kagame, Azam ni kubwa kwani inatetea ubingwa, kazi yetu ni moja kufanya vizuri na kutetea taji letu.

"Ninafurahi kwa sasa kuona timu ina muunganiko mzuri, wachezaji wanatambua kile ambacho ninawafundisha ni muda wa kufanya maajabu," amesema.

Leo Azam FC itamenyana na TP Mazembe kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali michuano ya Kagame inayoendelea nchini Rwanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic