KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars' kinatarajia kuingia kambini Julai 21 kujiandaa na michuano ya CHAN.
Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Stars, Ettiene Ndayiragije tayari ametangaza idadi ya wachezaji 26 ambao wataunda timu ya Taifa kwa ajili ya michuano hiyo.
Katika kikosi hicho wachezaji saba wametoka Azam FC, saba wengine Simba huku Yanga wakitoka wachezaji watano, KMC ikitoa wachezaji watatu, Polisi Tanzania, Coastal Union, U 17 na Namungo zimetoa mchezaji mmojammoja.
Stars itamenyana na Kenya Julai 28 uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment