July 21, 2019


BENO Kakolanya mlinda mlango wa Simba amesema kuwa msimu ujao watapambana kufikia malengo waliyojiwekea kutokana na aina ya kambi waliypo kwa sasa.

Simba ipo nchini Afrika Kusini na wanafanya mazoezi kwenye uwanja wa Royal Bafokeng Sports Complex mjini Rutenburg.

Kakolanya amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na matumaini yao ni kufanya makubwa msimu ujao.

"Kambi ipo salama na tunaendelea vizuri, ushirikiano uliopo unatujenga na kutupa imani ya kufanya vema msimu ujao," amesema.

Kakolanya ni mlinda mlango mpya ndani ya Sima atapambania namba na mlinda mlango namba moja Aish Manula.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic