ETIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa hakuna wanachofikiria zaidi ya ubingwa.
Azam FC imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuibamiza mabao 2-1 TP Mazembe kwenye mchezo wa robo fainali leo wana kazi mbele ya Manyema FC mchezo wa nusu fainali kombe la Kagame.
"Hakuna kingine ambacho tunakiwaza kwa sasa zaidi ya kucheza mechi mbili ambazo ni ya nusu fainali pamoja na fainali, na mpango mkubwa ni kutetea kombe letu," amesema.
Michuano ya Kagame inaendelea nchini Rwanda na Tanzania inawakilishwa na bingwa mtetezi Azam FC baada ya KMC kutolewa hatua za awali.
0 COMMENTS:
Post a Comment