July 15, 2019

UONGOZI wa Simba umesema kuwa malengo makubwa ni kuona timu zote mbili zinakuwa na ushindani msimu ujao wa 2019-20.

Ofisa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa mipango iliyopo ni kwa timu zote mbili kuanzia ile ya wanawake pamoja na ya wanaume kuleta ushindani.

"Ni malengo yetu kuona timu zote zinafanikiwa na kuleta ushindani kwenye michuano yote ambayo tutashiriki msimu ujao," amesema.

Timu ya Simba ya wanawake, Simba Queens imekwea pipa leo kuelekea nchini Ujerumani kwa ziara ya kisoka itakayochukua muda wa wiki mbili huku ile ya wanaume nayo ikikwea pipa kutimkia Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

2 COMMENTS:

  1. Migongo wazi wabakie na maneno.Simba tusonge mbele .Wenye majungu watachoka tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic