July 14, 2019


KOCHA wa makipa ndani ya Yanga, Peter Manyika amesema kuwa ameanza kazi na mlinda mlango Klaus Kindoki ambaye msimu uliopita mashabiki hawakumkubali kutokana na kufanya makosa mengi ya kiufundi.

Moja ya mechi ambayo Kindoki alifanya makosa ya kiufundi ni kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Stand United ambapo aliruhusu kufungwa mabao 3 na Alex Kitenge licha ya Yanga kushinda kwa mabao 4-3.

Akizungumza na Saleh Jembe, Manyika amesema kuwa ameangalia namna bora itakayomfanya awe katika ubora wake msimu ujao.

"Nimeanza na kuangalia namna bora ya kumrejesha kwenye ubora wake mlinda mlango Kindoki, msimu uliopita alifanya makosa mengi ya kiufundi hicho ndicho tunachokifanyia kazi, nina imani kwa programu ambayo wataifanya mambo yatakuwa safi," amesema.

Manyika amechukua nafasi ya Juma Pondamali ambaye amesema kuwa kwa sasa anataka kufanya kazi nyingine mbali na mpira.

2 COMMENTS:

  1. Yanga Mtake msitake uwekezaji mkubwa unatakiwa....michango ya wananchi/wanachama/mashabiki pesa za viingilio kwenye mechi, kuuza jezi hakuwezi kuwafanya kuwekeza kwenye miundo mbinu (kama ujenzi wa viwanja, akademi, hostel) na kusajili na kuwahudumia wachezaji wenye uwezo Africa, kuwa na benchi la ufundi la kisasa.....lazima mtafute wawekezaji 3 au 2. Pia preseason trials na timu za chini sio idea nzuri mashindano ya CAF yanakuja lazima friendly matches mpate zile zenye viwango vya juu....mnaweza mkafanya ziara katika nchi jirani....lakini sio kucheza na Nkamba Rangers au Mawenzi Market sio kipimo kizuri

    ReplyDelete
  2. Mambo ya Ngoswe muachie Ngowse mwenyewe wewe yanakuhusu na nini mambo ya Yanga Waachie Yanga wenyewe na viongozi wao wanajua nini wafanye si dhani kama wanataka ushauri wako huo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic