July 16, 2019


Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameshangaa kutokuona watanzania wakipewa nafasi ya kuifundisha Taifa Stars.

Kauli ya Julio imekuja siku chache mara baada ya Kocha Mrundi Ettiene Ndayiragije kuchaguliwa kukaimu nafasi ya Emmanuel Amunike aliyekuwa akiinoa timu hiyo.

Julio amemtaja Abdallah King Kibadeni kuwa mmoja wa makocha ambao wana heshima kuwa katika soka la Tanzania akipendelea wapewe nafasi hiyo.

Kocha huyo mwenye maneno mengi anaamini Kibadeni ambaye aliwahi kuinoa na kuichezea Simba pia anafaa kuinoa Stars kwa heshima aliyoiweka Tanzania .

"Nashangaa kwanini wazawa hawapewi nafasi.

"Tuna watu wengi ikiwemo King Kibadeni ambaye anaweza akachukua nafasi hiyo na akaifundisha Stars."

4 COMMENTS:

  1. Taifa stars ina makocha wawili wazawa na kwa kiasi fulani ndio wenye timu. Sasa madai mengine jamani ni ya kushangaza.

    ReplyDelete
  2. kibadeni sasa hivi anafundisha timu gani

    ReplyDelete
  3. Hata akipewa mzawa hamna kitu, TFF kwa kushirikiana na SERIKALI inatakiwa kwanza kuwekeza ktk soka la vijana, hao nao watafukuzwa tu.

    ReplyDelete
  4. TANZANIA HATUKUBORONGA
    Timu yetu ya Taifa kwangu Mimi haikuboronga,Tulichokifanya ni kikubwa kulingana tujipongezena kiwango chetu sasa na tuongeze juhudi AFCON ijayo tusogee hatua nyingine zaidi,sisi kufika fainali za AFCON huko ulikuwa ni hatua mbele. Waloboronga ni Misri kwani wao wamerudi nyuma.
    Sisi hatukutarajia makubwa zaidi ya kufika fainali hizo, kwa mafanikio hayo tuongeze juhudi zaidi.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic