KABLA HATA YA LIGI KUANZA, MBRAZIL SIMBA AANZA NA YANGA
Beki mpya wa Simba kutoka Brazil, Gerson Fraga amesema kuwa anatamani msimu mpya uanze haraka ili aoneshe kile alichonacho.
Akizungumza mara baada ya kutua nchini Afrika Kusini ambapo kikosi cha Simba kimeweka kambi maalum kujiandaa na msimu ujao, ameelezea matamanio yake ya kucheza Ligi Kuu Bara.
Fraga amefunguka kuwa anatamani zaidi pia kucheza mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga baada ya kupata taarifa kuwa ndiyo wapinzani wakubwa wa Simba hapa nchini.
Aidha, Fraga amesema ni jambo kubwa kuwa na la furaha kwake kuwa na Simba huku akiwasifia mashabiki wa timu hiyo kwa namna walivyompokea.
0 COMMENTS:
Post a Comment