July 20, 2019

ZANA Coullibary mzee wa kumwaga na kumimina maji sasa ni wazi msimu ujao atakuwa ndani ya kikosi cha Namungo FC endapo dili litakamilika akitokea Simba.

Kocha wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema kuwa mipango ya usajili inaendelea hivyo wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa.

"Tupo sawa kwa ajili ya msimu mpya na kazi yetu ni kusajili wachezaji wenye uzoefu ambao watatuletea mafanikio.

"Suala la Zana, bado dili halijakaa sawa mipango ikikamilika tutaweka kila kitu wazi kwani timu yetu ipo imara," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic