KAGERE AKIMBILIA GYM
Wakati Yanga wakianza mazoezi ya pamoja Jumatatu iliyopita kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, mshambuliaji wa Simba Mnyarwanda, Meddie Kagere naye ameanza kufanya programu binafsi ya gym pekee.
Yanga imeingia kambini Jumatatu ikiwa na wachezaji wake wa zamani na wapya ambao wamesajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 23, mwaka huu.
Baadhi ya wachezaji wapya walioingia kambini mkoani Morogoro na kuanza mazoezi ni beki Mghana, Lamine Moro, Mustapha Suleimani, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Abdulaziz Makame na Muharami Salumu ‘Marcelo’.
Kagere alisema tayari ameanza mazoezi binafsi tangu Jumanne mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi.
Kagere alisema kuwa, programu aliyoanza nayo hivi sasa ya gym ni kwa ajili ya kutengeneza fitinesi ya mwili, baada ya kutoka mapumzikoni na lengo ni kuwa fiti kabla ya kuanza yale ya pamoja kitimu.
“Nimewahi kurejea jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupata muda wa kupumzika na kuanza programu ya pekee ya kufanya mazoezi kabla ya kuanza ya kitimu pamoja na kocha.
“Lengo ni kuwa fiti mapema huku nikiwasubiria wenzangu waliokuwa mapumzikoni ili tutakapoungana kuanza mazoezi mimi niwe fiti zaidi yao.
“Ninataka kuona msimu ujao ninakuwa fiti zaidi ya msimu uliopita na hilo linawezekana kwangu na kikubwa ni kuendelea kuipa mafanikio ya makombe likiwemo hili la ligi,” alisema Kagere
mzee wa kazi huyo anajua anachokifanya, wengne utasikia wanamatatizo ya kifamilia
ReplyDelete