TAMBWE AMPA MAAGIZO ZAHERA
Amis Tambwe amepaza sauti kutoka Burundi hadi Tanzania akimtaka Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amrudishie kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yondani.
Yondani alipewa kitambaa cha unahodha kwenye mechi za maandalizi za msimu uliopita baada ya beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu lakini baadaye Yondani alivuliwa kwa madai ya utovu wa nidhamu.
“Tusubiri tuone kama Zahera atakubali ushauri kuhusu hili la kumrudishia Yondani kitambaa japokuwa nafahamu ana misimamo yake na kila mtu anaijua, hakuna mchezaji anayestahili kuwa nahodha zaidi ya Yondani.”
“Kwanza kabisa ni mchezaji mzoefu lakini pia kwa sasa ndiye mchezaji mkongwe katika kikosi hicho kuliko wengine wote na ana heshimika na kila mchezaji kutokana na uwezo wake uwanjani.”
Tambwe unajihangaisha bure utafute timu nyengine kama alivofanya mwenzio Haruna tena bila ya kuchelewa Yanga imeshasheheni nyota WA kila aina
ReplyDeleteau akajiunge na timu ya netball maana anajua sana kufunga kwa mkono mpira wa miguu hana kitu ndio maana hawajamuita timu ya taifa
ReplyDeleteHayo ni maoni yke
ReplyDelete