July 21, 2019



RATIBA ya awali ya Ligi ya Mabingwa imetoka ambapo wawakilishi wa Tazania Simba na Yanga wamezijua timu watakazoanza nazo.


Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wataanza kucheza na UD DO Sonso ya Msumbiji mchezo wa kwanza utachezwa kati ya Agosti 9/10/11 mwaka huu nchini Msumbiji huku ule wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23/24/25 jijini Dar.

Yanga itaanza kumenyana na Township rollers nchini Botswana na mchezo wa marudiano utapigwa Dar kisha mshindi wa mchezo huo atamenyana na mshindi kati ya  Zesco na Green Mamba.

3 COMMENTS:

  1. Haya mazoezi ya Simba ndio maandalizi sio Yanga wao mbio tu.....ratiba ya CAF CL imetoka timu zijiandae kama inavyofanya Simba ili nafasi ya kuingiza timu 4 tusizipoteze....nina mashaka sana na Yanga naona hawako makini Township Rollers waliyopangiwa ni timu ngumu sana wasijekuishia raundi za awali....maana kama akipita hapo Zesco ya Zambia inamsubiri.....naona Tanzania tutapoteza zile nafasi 4 ikiwa moja ya timu zetu zitatolewa mechi za raundi ya awali

    hili ni tatizo kubwa kwa timu zetu zikiwemo za za Taifa na haswa Vilabu vinavyowakilisha kwenye mashindano ya kimataifa"kuyaficha"madhaifu yetu....halafu uhalisia unaonekana kwenye matokeo kupigwa 3 ama 5.....maandalizi yetu mara nyingi ni duni na ya hali ya chini mno...ila hatutaki kuambiwa ukweli ili tujirekebishe

    ReplyDelete
  2. Sahihisha hapo kwani Yanga inaanzia ugenini na si Dar es salaam

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic