July 22, 2019


PETER Manyika, kocha wa makipa wa timu ya Yanga amesema kuwa kwa namna ubora wa makipa wake ulivyo atakayekuwa bora ndiye atakayeanza kikosi cha kwanza.

Manyika amesema kuwa amewatazama makipa wake watatu ambao amefanya nao mazoezi na kukubali uwezo wao na anatarajia kuanza kufanya kazi na kipa mpya, Farouk Shikalo ambaye amewasili nchini jana.

"Kwa idadi ya makipa ambao ninao kwa sasa, atakayeanza kikosi cha kwanza ni yule mwenye juhudi na nguvu za ushawishi kwani tayari wote nimewajenga.

"Nilianza na Kindoki ambaye msimu uliopita alifanya makosa ya kiufundi nimemgundua, msimu ujao atatisha, hao wegine nina amini uwezo wao hivyo atakayekuwa na jitihada ndiye atakayeanza,"amesema.

Sasa Yanga ina makipa wakali wanne ambao ni pamoja na Klaus Kindoki, Metacha Mnata, Farouk Shikalo na Ramadhan Kabwili.

1 COMMENTS:

  1. Yanga leteni wawekezaji hamuwezi kuwa na timu imara bila uwekezaji haya mengine ni porojo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic