BAADA ya
kocha wa timu ya KMC, Jackson Mayanja kupewa kandarasi ya mwaka mmoja ndani ya
kikosi hicho ambacho kitashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao amepewa
jukumu la kumleta msaidizi wake kwenye benchi la ufundi.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa anajua kwamba anawatambua makocha
wengi wenye uzoefu hivyo atafanya nao mawasiliano kwa ukaribu kwa kushirikiana
na uongozi wa KMC ili kupata kilicho bora.
“Mpango
wangu mkubwa ni kumleta msaidizi makini ambaye tutafanya naye kazi kwa
kushirikiana, kwa sasa tayari nimepewa baraka na uongozi hivyo ni muda wangu
kutafuta mtu wa kufanya naye kazi kwenye benchi la ufundi,” amesema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment