IMEELEZWA
kuwa mshambuliaji wa Mwadui FC, Salim Aiyee ameipasua timu yake kwa sasa
kutokana na kusepa kwake na kujiunga na
KMC na kukikacha kikosi cha Mwadui ambacho ni miongoni mwa timu 20
zitakazoshiriki Ligi Kuu Bara.
Habari
kutoka ndani ya Mwadui FC zimeeleza kuwa tayari uongozi wa Mwadui FC umeanza mazungumzo na nyota wa Mbao FC Said Jr ili kuziba pengo la Aiyee.
“Mwadui kwa
sasa wanahaha kumpata mbadala wa Aiyee ambaye msimu ujao atakipiga KMC, hesabu zao ni kumpata mshambuliaji mwingine atakayeziba pengo
lake na jicho kubwa kwa sasa lipo kwa Said Jr wa Mbao FC,” kilieleza chanzo
hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment