UWANJA wa Al Salam leo nchini Misri wanaume 22 watazitikisa nyasi kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Afcon.
Nigeria itamenyana na Tunisa ambao wote walipoteza kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali iliyochezwa Jumapili.
Tunisia ilipoteza mbele ya Senegal kwa kufungwa bao 1-0 huku Nigeria wakipoteza mbele ya Algeria kwa kufungwa mabao 2-1.
Zimekutana mara nne ambapo Nigeria imeshinda michezo mitatu huku Tunisiia wakiambulia ushindi mara moja.
1978 katika mji wa Accra Ghana, Nigeria ilipewa ushindi wa mabao 2-0 baada ya Tunisia kususa wakidai kuwa walikuwa wanaonewa na mwamuzi na kabla ya kutoka uwanjani wote walikuwa wamefungana bao 1-1 na kwa kosa hilo mwaka unaofuatwa Tunisia ilifungiwa kushiriki Afcon.
2000 zilikutana kwenye michuano hiyo hatua ya makundi ambapo Nigeria ikashinda kwa mabao 4-2 nchini Nigeria na 2004 Tunisia iliifunga Nigeria kwa penalti 5-3 nusu fainali baada ya dakika tisini kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 nchini Tunisia.
2006 walimenyana nchini Misri mchezo wa robo fainali na Nigeria ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya dakika tisini kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment