UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa kwa wachezaji wote wenye vipaji na wanajua kucheza mpira ni zamu yao kujitokeza leo kwa wingi uwanja wa Mabatini ili kuanza mchujo kwa gharama zao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa ni fursa kwa kila mchezaji kuonyesha uwezo wake na atakayepenya atasajiliwa moja kwa moja.
"Tunaanza leo asubuhi kufanya mazoezi ambapo yatakuwa ni kwa muda wa siku tatu, muda ni kuanzia saa mbili asubuhi mwisho itakuwa Alhamisi na lengo ni kupunguza gharama za usajili," amesema .
0 COMMENTS:
Post a Comment