SIMBA KUCHEZA KWENYE MIJI MITATU SAUZI
SIMBA ambayo ipo kambini nchini afrika Kusini ambapo inatajwa kambi hiyo ni ghrama kubwa, imetangaza kuwa itacheza michezo mitatu ya kujipima nguvu. Kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na kambi ya Simba huko Afrika Kusini, huku Watanzania wanaoishi nchini humo wakihoji timu hiyo imepata wapi fedha za kukaa kwenye kambi ya kisasa namna hiyo.
Simba wameweka kambi sehemu moja na mabingwa wa zamani wa Afrika, Orlando Pirates ikielezwa kuwa ni jeuri ya mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed dewji ‘Mo’ ambapo taarifa zinadai, moja ya mechi ya kirafiki itakayocheza Simba, itakuwa dhidi ya timu hiyo.
Wakati nyota wa kikosi hicho wakifika Afrika Kusini juzi Jumatatu na kuanza maandalizi ya msimu ujao, baadhi ya nyota wengine wa kikosi hicho akiwemo Deo Kanda, Sharaf Eldin Shiboub, Francis Kahata na Meddie Kagere, wanatarajia kuwasili nchini humo leo Jumatano baada ya taratibu za kuwapatia visa kukamilika.
Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe, amesema kuwa, kikosi hicho kinatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki katika miji mitatu tofauti.
“Simba itacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya timu ya Cape Town Football Club itakayocheza baada ya mazoezi ya awali, tukimaliza hapo itacheza mechi nyingine mbili kwa mujibu wa matakwa ya kocha Patrick Aussems ambazo uongozi unaendelea kufanya mazungumzo.
“Timu zitatoka katika miji mitatu tofauti ambapo ni Gutenberg, Cape Town na Pretoria, hivyo kikosi kitapata wasaa wa kujiandaa ipasavyo kabla ya kurejea kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day,” alisema Kashembe.
Isionekane ajabu pesa za Simba za hoteli na usajili ghali zimetoka wapi wakati inajulikana na kila MTU zitokako lakini badili yake istaajibike pesa za usajili za watani zatoka wapi wakati Hali ngumu Yao inajulikana
ReplyDelete