August 4, 2019


WAYNE Rooney, nyota wa zamani wa Manchester United amesema kuwa malengo yake makubwa ni kuja kuwa Kocha wa kikosi cha United atakapostaafu Soka.

United Kwa sasa ipo chini ya mchezaji wa zamani wa kikosi hicho Ole Gunnar Solskjaer.

Rooney mwenye umri wa miaka 33 kwa sasa anakipiga ndani ya DC United mpaka mwaka 2020 ila amesema anatazama matarajio yake ya baadaye.

Chanzo cha karibu na Rooney kimeeleza kuwa :"Wayne Kwa sasa anaangalia malengo yake ya baadaye na bado anapenda kuwa kwenye mpira hivyo anaitazama familia yake na mambo mengine.


 "Anaitazama United kama sehemu yake sahihi anapenda siku moja awe kocha wa kikosi chake cha zamani, muda mrefu sana anapenda kuwa sehemu ya Ole kwa vitendo,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic