SHOMARI Kapombe, beki wa Simba amesema kuwa kwa sasa yupo fiti na anaimani ya kufanya vizuri ndani ya Simba kwenye michuano ya kitaifa na kimataifa.
Kapombe alikuwa anasumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu kwa sasa amerejea kwenye ubora wake na alikuwa ni sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo ya Zambia ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.
Kapombe amesema kuwa,:" Tupo sawa na kila kitu kinakwenda vizuri, nashukuru nimerejea kwenye ubora wangu ni jambo jema na ninaamini tutafanya makubwa msimu huu kitaifa na kimataifa.
"Sapoti kubwa mashabiki ambayo wamekuwa wakitupatia Simba iwe ya kudumu kwani kwa kufanya hivyo kunatupa morali ya kupambana zaidi," amesema.
Kapombe ameongeza kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba ni miongoni mwa wachezaji waliotia fora siku ya Simba Day kwa kupokewa kwa shangwa na mashabiki Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment