MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hana mashaka na kikosi alichonacho kwa sasa kwani kitampa matokeo chanya kimataifa.
Yanga Jumamosi itakuwa uwanja wa Taifa ikicheza mchezo wa awali dhidi ya Township Rollers kabla ya kurudiana nao ugenini kati ya Agosti 23-25.
Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa anaona namna kikosi kinavyopambana na anaimani kwamba kitapata matokeo chanya kwenye michezo ya kimataifa.
"Kwa hapa ambapo kikosi kimefikia sio sehemu mbaya kwani kila mmoja ana morali ya kufanya kazi na kutimiza majukumu yake uwanjani.
"Tunajua kwamba tuna kazi ya kucheza kimataifa hilo halitupi taabu tumejiandaa na mashabiki watupe sapoti ili tufanye vizuri," amesema.
Yanga kwa sasa imeweka kambi visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandaliz ya mwisho ya mchezo huo na inatarajiwa kurejea muda wowote kuanzia sasa Bongo.
Lakini hiyo Rollers Ni timu ngumu Sana kuliko Ile ya Mlandege kwahivo inahitaji hadhari kubwa Sana na tuombe Mungu
ReplyDelete