August 7, 2019


LEO Jumatano saa 10 alfajiri kikosi cha Azam FC kinatarajia kuanza safari kuelekea nchini Ethiopia kwa ajili ya kuiwahi  Fasil Kenema kwenye mchezo wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Bahir Dar Jumapili saa 10.00 jioni.

Msafara wa Azam FC utaondoka na wachezaji 23,watano wa benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije pamoja na viongozi na maofisa wa timu hiyo.


Mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports watakaoondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia, wamejipanga vilivyo kufanya vema kwenye michuano hiyo msimu huu, ikiwa na malengo ya kufika hatua ya makundi. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic