August 16, 2019



UONGOZI wa KMC, umeamua kutumia mtindo wa Simba katika kuhamasisha mashabiki wake kuelekea kwenye mchezo wa kimataifa wa kombe la Shirikisho dhidi ya AS Kigali ya Rwanda unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa Taifa kati ya Agosti 23-25 kwa kuja na kauli mbiu ya ‘Together we Can’.

Simba msimu uliopita kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa  walikuwa wanatunga kaulimbiu maalumu kwa ajili ya hamasa huku ile ya 'Yes We Can' ikiwa ni moja ya iliyobamba na zilikuwa zinatambulishwa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa wameamua kuja na kauli mbiu ili kuongeza hamasa na nguvu ya mashabiki kuelekea kwenye mchezo  wa marudiano.

“Utakuwa ni mchezo mgumu na tayari kikosi kimeanza mazoezi kujiaandaa kuwavaa AS Kigali, tumeamua kuja na kaulimbiu ya ‘Together we Can’  ili kuongeza hamasa na nguvu kwa mashabiki kuelekea kwenye mchezo wetu.

“Ombi letu mashabiki wajitokeze kwa wingi washuhudie namna wachezaji watakavyotoa burudani na kuwapa furaha kwa kupata matokeo chanya kwani kila kitu kinawezekana,” amesema Binde.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic