August 13, 2019


JUMA Pondamali, aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Yanga amesema kuwa kwa sasa atapambana na muziki kuufikisha hatua za kimataifa.

Pondamali kwa sasa amekacha kazi ya mpira na badala yake amegeukia muziki akiwa ni msimamizi, mwandishi na mwimbaji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Pondamali amesema kuwa amefanya uchunguzi wa kutosha na kuona kwamba muziki una nafasi kubwa ya kumtoa kwenye maisha.

"Naifanya hii kazi haimanishi nimeanza leo nimeanza muda mrefu sana na nimetunga nyimbo nyingi za Yanga ambazo hazikupata umaarufu mkubwa kutokana na kutokuwepo na matamasha kama ambavyo wapinzani wetu walikuwa wanafanya.

"Muziki ambao nasimamia na kufanya ni Singile huku ndiko ambako nitafiti hivyo mipango mingi inakuja na nyimbo kali zinakuja, lengo kubwa ni kuvuka hatua ya kitaifa mpaka kimataifa" amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic