UONGOZI wa
Lipuli umesema kuwa kwa sasa hauna hesabu za kubeba kombe la Ligi Kuu Bara
ambalo lipo mikononi mwa mabingwa watetezi Simba.
Simba
ilitwaa ubingwa misimu miwili mfululizo baada ya kuchukua mikononi mwa
Yanga msimu wa mwaka 2017/18 na kutetea tena kwa msimu wa mwaka 2018/19.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Lipuli FC, Festo Sanga amesema kuwa
mpango mkubwa wa timu ya Lipuli kwa sasa ni kuleta ushindani wa kweli na sio
kutwaa kombe.
“Tunatambua
kwamba kila timu ina mipango yake nasi pia hatupo nyuma, mpango mkubwa ni kuwa
kwenye nafasi nne za juu kisha wakati mwingine tutajipanga kutwaa kombe.
“Kila kitu
kinakwenda sawa tunashosubiri ni ligi kuanza ndipo tutaonyesha kile
tulichonacho, nafasi ambayo tunaitaka sana ni nafasi ya tatu msimu ujao,”
amesema Sanga.
Lipuli FC
msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23 itamkosa kocha wao Seleman Matola
ambaye kwa sasa anainoa timu ya Polisi Tanzania.








0 COMMENTS:
Post a Comment