August 13, 2019


 BENO Kakolanya mlinda mlango mpya wa Simba ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwli akitokea Yanga amemkosha, Patrick Aussems kutokana na uwezo wake.

Kakolanya alianza kwenye mchezo wa kwanza wa kimataifa hatua ya awali dhidi ya UD Songo nchini Msumbiji na hakuruhusu nyavu zake kuguswa licha ya kukumbwa na hatari nyingi langoni mwake.

Aussems amesema: “Kakolanya anafanya vizuri, sina wasiwasi tena kama ilivyokuwa msimu uliopita nilivyokuwa nikipata taabu pindi Manula akiumia.

“Mechi zote alizocheza amefanya vizuri kwa hiyo ni matumaini yangu kuwa kadiri siku zinavyoenda atakuwa bora zaidi na atatoa changamoto kubwa Manula," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Apewe nafasi ya kudaka zaidi hata baada ya Manula kurejea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic