August 7, 2019


KIUNGO wa Wolves, Morgan Gibbs-Whites msimu uliopita alikuwa kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 9.
Kinda huyo anayekipiga Wolves ana umri wa miaka 19 tu na ameshaanza kupata uzoefu wa kucheza mechi kubwa na ngumu ndani ya Premier League.
Msimu uliopita alicheza jumla ya mechi 26 na ameanza kwenye jumla ya mechi saba ambazo zote alizimaliza na alikuwa anahusika kwenye maandalizi ya mechi za Ligi ya Europa.
Ni zao la timu ya vijana ya Wolves ambayo imemkuza na kumfanya awe na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutoa pasi zenye uhakika kwa nafasi ambayo anaicheza kwa sasa.
Ameongeza ujasiri na uwezo baada ya kuaza kwenye mchezo wa maandalizi ya msimu ujao dhidi ya Newcasstle United ambapo alipata bahati ya kufunga bao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic