NAHODHA
msaidizi wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Juma Kaseja amesema kuwa bado
kuna kazi kubwa ya kufanya kwa mashabiki ili kusonga mbele kwenye michuano ya
Chan.
Tanzania
imepenya hatua ya awali ya michuano ya Chan baada ya ushindi wa penalti 4-1
dhidi ya Kenya kwenye mchezo wa marudio uliochezwa nchini Kenya ambapo Kaseja
aliibuka shujaa kwa kuokoa penalti moja.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa kila kitu kwenye mpira kinawezekana
hivyo kazi kubwa kwa mashabiki ni kuendelea kuipa sapoti timu mwanzo mwisho.
“Hakuna
kikubwa ambacho kinatufanya tupate matokeo chanya zaidi ya nidhamu na juhudi
ndani ya uwanja hivyo kazi ya kwanza ikiisha inafuata kazi nyingine, nawaomba
mashabiki waendelee kutupa sapoti ili tufanye vema.
“Kitu cha
kwanza ambacho kinapaswa kipewe kipaumbele ni Taifa kwanza kisha mengine
yatafuata wachezaji ni jukumu letu kufanya kile ambacho kina manufaa kwa Taifa
na mashabiki pia waendelee kuwa pamoja nasi,” amesema Kaseja.
0 COMMENTS:
Post a Comment