August 8, 2019


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohammed Dewj 'Mo' amesema kuwa anapenda kuona timu ya Simba inafikia hatua kubwa ya mafanikio kitaifa na kimataifa.

Mo amesema kuwa mpango ambao upo kwa sasa kati ya uongozi ni kuirejesha timu mikononi mwa watu ili nao wawe sehemu ya historia ya mafaniko ya kikosi hicho.

"Naipenda timu ya Simba na ninawapenda mashabiki pia wa Simba, kwa sasa tunafanya mchakato kuwafanya wananchi wawe sehemu ya mafanikio ya Simba kwa kuwaruhusu nao wachangie fedha kwa ajili ya kkamilisha shughuli za maendeleo ya Simba ikiwa ni pamoja na ujezi wa uwanja wa Bunju pamoja na mambo mengine.

"Maono yetu kwa pamoja ni kuona Simba inafikia hatua kubwa ya uwekezaji kama ambavyo wenzetu wanafanya nje kwani nimejifunza mambo mengi nilipokuwa huko na ni wakati wa kuona kwamba kila mmoja anakuwa sehemu  ya mafanikio," amesema Mo.

10 COMMENTS:

  1. Safi sana Mo kwani kwa mfano elimu bure basi tena mzazi hana haki ya kuchangia maendeleo ya mwanae shuleni? Waswahili wanasema abebwae hapaswi kujiachia.

    ReplyDelete
  2. Safi sana watanzania tubadilike tutumie sapoti kusogea mbele zaidi siyo kuwaachia wadhamini Kama tunakimbi 10km/hr basi tukipata saport tuongeze speed iwe kubwa zaidi

    ReplyDelete
  3. Nasikia vyura wamepata milioni 280 wakati next level wamepata milioni 700!!Mwenye mipango mizuri anaeleweka.Kelele nyingi bila mipango mizuri ni upotevu wa muda.

    ReplyDelete
  4. Chaajabu nao wanadai Waliujaza uwanja.au waliingia bure? mi sielewi

    ReplyDelete
  5. Asilimia 51 ya hisa wanazo wanachama kwa hiyo lazima wanachama waje na mchango wao.Kama Una makamasi kwenye ubongo ndio utashindwa kuelewa. Simba ni timu ya WATU.

    ReplyDelete
  6. yanga walsemwa sana khs uchangishaj leo kko wapi ukiona mwenzio ananyolewa zako tia maji na uctake mamba kabla hujavuka mto bakuli part 2 halkwepek

    ReplyDelete
  7. Tofauti Simba hawachangii kulipa mishahara nä pesa za usajili .Wanachama wananunua hisa ili kupata faida kwenye uwekezaji wao.Ndio maana huoni bakuli.Ununuaji utaanza tarehe 1 September 2019.Wacha kulinganisha mlima na kichuguu .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bora umemjibu huyo wa juu yako. Maana anaonekana hana uwezo wa unyumbulifu wa mambo.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic