PHIL Foden, kiungo mshambulijaji ni miongoni mwa nyota wenye kipaji cha hali ya juu ambacho wapo nacho kati ya wachezaji vijana ambao wanakipiga Ligi Kuu England.
Nyota huyu anakipiga Manchester City ana umri wa miaka 19 na msimu uliopita alicheza jumla ya michezo 25 na timu yake ilitwaa ubingwa kati ya hiyo ni mitatu tu alianza.
Mpaka sasa amebaki ndani ya kikosi cha Manchester City huku meneja, Pep Guardiola akimuamini kwa kiasi kikubwa na anataka kumuona akifika mafanikio makubwa msimu ujao.
Pia anakipiga kwenye timu ya Taifa chini ya miaka 21 ya England anaandaliwa kuwa mrithi wa David Silva kwa ajili ya msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment