SELEMAN Matola, Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa ushindani msimu ujao utakuwa mgumu kutokana na timu zote kujipanga kwa ushindani.
Matola amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwa timu nyingi kujipanga kiushindani licha ya kutototangazwa kwa mdhamini mkuu.
"Ushindani msimu ujao utakuwa mkubwa na kila timu imejipanga, ila changamoto kubwa ambayo ipo kwa sasa ni kwa upande wa mdhamini mkuu kwani mambo bado.
"Endapo atapatikana mdhamini ligi itanoga kwani timu nyingi kwa sasa zinajiendesha zenyewe na hali sio shwari kiuchumi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment