LEO kimataifa ni zamu ya Azam FC kurusha kete ya
kwanza hatua ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Triangel United ya
Zimbabwe.
Sasa kwa
wakazi wote wa Dar es Salaam na viunga vyake kazi ni moja tu kuipa sapoti timu
ya Azam FC ambayo itakuwa kwenye uwanja wake wa Chamazi Complex.
Ile nguvu ya jana pale uwanja wa Taifa wakati Yana ikimenyana na Zesco basi ihamie kwa wa Kimataifa wengine Azam FC.
Azam Kimataifa
Imepanda
ligi mwaka 2008 imeanza kushiriki michuano ya kimataifa mwaka 2013 mpaka sasa
kwenye uwanja wa Chamazi imecheza jumla ya michezo tisa ya kimataifa katika
hiyo imeshinda saba na kutoa sare miwili.
Rekodi
zinaonyesha uwanja wa Chamazi mpaka sasa kwenye jumla ya michezo tisa ya kimataifa
Azam wamefunga jumla ya mabao 15 huku wao wakifungwa sita,
Hizi hapa za kimataifa zilinyoooshwa
Chamazi
Azam FC
3- 1 El Nasir ya Sudan, Azam FC 1-0 Ferroviarioda Beira ya Msumbiji, Azam FC
2-0 Al-Merrik ya Sudan, Azam FC 4-3 Bidvest ya Afrika Kusini, Azam FC 2-1
Esperance de Tunis ya Tunisia, Azam FC 1-0 Mbabane Swallow ya Eswatin na Azam
FC 3-1 Fasil Kenema ya Ethiopia.
Hizi hapa kimataifa zililazimisha
sare
Azam FC 0-0
Barrack Young hii ni timu kutoka Liberia, Azam FC 0-0 FAR Rabat ya Morroco ni
hizi mbili zilikuwa na kismati ndani ya uwanja wa Chamazi.
Wachezaji watakaokosekana
Agrey Morris
nahodha wa Azam FC anaendelea na matibabu ya goti. Kiungo Mudhathir Yahya
tayari ameanza mazoezi na wenzake alikuwa anasumbuliwa na goti ni suala la muda
tu kuanza leo.
Mapilato ni majirani zetu
Mchezo wa
leo utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni na mageti kwa sasa yapo wazi, mapilato watakaoamua mchezo waliwasili jana kutoka kwa
majirani zetu hapo anapotokea nyota wa Simba, Meddie Kagere nchini Rwanda.
Uchakavu sasa
Tiketi ni
buku tatu kwa majukwaa ya mzunguko,
5,000 kwa majukwaa ya daraja la kati na V.I.P nyekundu moja tu (10,000) huku
kukiwa na zawadi ya Ukwaju pamoja na juice mpya ya Ukwaju bila kusahau Ice
Cream.
Umuhimu wa mchezo wa leo
Mechi ya leo
kwa Azam FC ni muhimu kimataifa kwani wakishinda kwa mabao mengi wanajiweka
kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele hatua inayofuata kwa kufuzu hatua ya
mwisho ya mtoano ‘play off’ na itacheza na moja ya timu 16 zilizotolewa kwenye
raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika zikitafutwa timu 16 zitakazopangwa
kwenye makundi manne ya Kombe la Shirikisho.
Hili hapa kosi la ushindi
Razak
Abalora yupo langoni kwa upande wa mabeki
Nickolas
Wadada, Bruce Kangwa,Daniel Amoah na Yakubu Mohamed twende kwenye viungo,Richard
Djod, na Salum Aboubakar ‘Sure boy’ washambuliaji Obrey Chirwa, Donald Ngoma,
Emmanuel Mvuyekule na Idd Seleman ‘Naldo’.
Hawa
watakuwa wanausoma mchezo nje,Mwadin Ally, Oscar Masai, Abdallah Masoud, Salmin
Hoza, Frank Domayo, Paul Peter, Idd Kipagwile.
Etienne Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema :“Ni mchezo mgumu na
muhimu kwetu kushinda, kila kitu kipo sawa na tuna amini tuna nafasi ya
kushinda ukizingatia tupo nyumbani kikubwa ni sapoti ya mashabiki na wachezaji
watatimiza majukumu yao,”.
Kila la kheyr Azam
ReplyDelete