September 15, 2019



MIRAJ Athuman, nyota mpya wa Simba ambaye amesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Lipuli amesema kuwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems amempa jukumu la kufunga kila akiwa uwanjani.

Miraj amefunga jumla ya mabao mawili kwa sasa kwenye michezo yake miwili ambayo amecheza ndani ya Simba alianza kufungua akaunti mbele ya JKT Tanzania na la pili alifunga mbele ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza na Saleh Jembe, Miraj amepewa jukumu la kucheka na nyavu kila akipewa nafasi ndani ya Simba.

"Jukumu langu kwa nafasi ambayo nacheza napaswa kucheka na nyavu muda wote na ndicho ambacho Kocha huwa ananiambia kila ninapokuwa benchi ama wakati naingia ndani ya uwanja," amesema.

Simba imejikusanyia jumla ya pointi sita kwa sasa ikiwa imefunga jumla ya mabao matano na imeruhusu kufungwa mabao mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic