UONGOZI wa
Azam FC umesema kuwa kwa sasa umeanza kazi ya kuinoa safu yao ya ushambuliaji
inayoongozwa na Obrey Chirwa pamoja na Donald Ngoma kuelekea kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Triangle United.
Azam FC inapeperusha bendera ya Taifa kwenye michuano ya kimataifa ilianza vibaya
kwenye mchezo wa kwanza mbele ya Triangle FC hatua ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho uliochezwa uwanja wa Azam Complex
kwa kukubali kufungwa bao 1-0.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wameanza kufanyia kazi mapungufu waliyoyaona kwenye mchezo wao wa kimataifa.
“Tulipoteza
mchezo wetu wa kwanza kutokana na kushindwa kwa washambuliaji wetu kuwa na
mbinu mbadala ambazo zingetupa matokeo, tumeona namna walivyokosea na
tumejifunza kwa sasa tunafanyia kazi.
“Ni makosa
madogo ambayo yametugharimu lakini huu ni mpira na tunajua kwamba yote ni
matokeo, kama wao wameshinda hapa basi nasi tunakwenda kushinda kwao, Ngoma na
Chirwa watanolewa upya pamoja na wachezaji wengine,” amesema Cheche.
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Septemba 28 nchini Zimbabwe na ili Azam FC isonge mbele ni lazima ishinde kuanzia mabao 2 kuendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment