UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa moto wao msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara haupoi mpaka
watakapoipoteza Mbao kwenye ramani jumla wakikutana.
Kagera Sugar
msimu huu imeanza kwa kukusanya pointi sita za mapema
kwa kushinda mbele ya Biashara United na Alliance FC, jumapili watakuwa mzigoni
wakimenyana na Mbao FC uwanja wa CCM Kirumba.
Akizungumza
na Championi Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa
hawatatulia kwa kasi waliyoanza nayo mpaka kitakapoeleweka mbele ya Mbao FC.
“Tumeanza
vizuri kutokana na maandalizi ambayo tuliyafanya, kwa sasa bado tunaendelea
kujiweka sawa ili kupata matokeo chanya kwenye michezo yetu inayofuata kwani
kila kitu kinawezekana.
“Ushindani
ndani ya ligi ni mkubwa nasi tunajitahidi kupata kile ambacho mashabiki na timu
tunahitaji kikubwa ni sapoti ya mashabiki katika kile ambacho tunakifanya kwa
sasa,” amesema Maxime.
0 COMMENTS:
Post a Comment