JUMA Mgunda,
Kaimu Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania inayojiaandaa na mchezo wa
kimataifa wa michuano ya Chan dhidi ya Sudan amesema kuwa hakuna wapo tayari kupata ushindi.
Stars kwenye
michuano hii ya wachezaji wa ndani itarusha kete yake ya kwanza Jumapili na
tayari timu imeanza maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa wachezaji wanatambua kazi yao kubwa ni kutafuta matokeo na wapo tayari kwa hilo.
“Mapungufu
ambayo yalikuwepo awali hasa kwenye safu ya ushambuliaji ndiyo tunayafanyia
kazi kwa ukaribu kwani ili timu ishinde ni lazima ipate mabao mengi kwa kuwa
tunaanza nyumbani basi tunapambana kupata matokeo chanya,” amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment