September 14, 2019


KOCHA Msaidizi wa Azam FC Idd Cheche amesema kuwa jukumu la kuwamaliza mapema wapinzani wao Triangel United Jumapili uwanja wa Chamazi ipo mikononi mwa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Obrey Chiwa pamoja na Donald Ngoma.

Chirwa na Ngoma waliwahi kuitumikia timu ya Yanga kwa nyakati tofauti kabla ya kuibukia ndani ya Azam FC kwa sasa.

Azam FC kesho itakuwa uwanja wa Chamazi ikimenyana na Triangle United ya Zimbabwe kwenye mchezo wa hatua ya  Kwanza wa Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa ili timu ishinde ni lazima washambuliaji wafanye kazi yao mapema jambo ambalo wamekuwa wakilifanyia kazi kwa muda mrefu kutokana na matatizo ya kikosi.

“Siku zote mwalimu anafanya kazi ya kurekebisha makosa yalipo na tatizo kubwa awali lilikuwa kwenye safu ya ushambuliaji kwa upande wa ulinzi huko tupo vizuri sasa tayari tumeshawapa majukumu washambuliaji wetu.

“Kwenye mchezo wetu wa kwanza nyumbani tunahitaji ushindi wa mabao mengi tena tumewaambia washambuliaji wafunge mabao ya mapema, jukumu la kufunga pia tumeliweka kwa timu nzima ili kurahisisha kazi mbele ya wapinzani, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Kwenye michezo miwili ya Kimataifa dhidi ya Fasil Kenema, safu ya ulinzi iliyo chini ya Yakub Mohamed iliruhusu mabao mawili pekee huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao matatu yalioivusha hatua ya awali.

1 COMMENTS:

  1. Kila la heri wana wa nyumbani chamazi wamalizeni hao kimya kimya wacha wapayukaji waendelee kucheza mpira mdomoni mwisho dakika 90.Watajua nimdomo au mguu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic