MIRAJ Athuman, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgij, Patrick Aussems alimpa maelekezo maalumu wakati anaingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Hassan Dilunga kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar.
Miraj alifunga bao la ushindi dakika ya 68 akimalizia pasi ya Shiboub kwa kupiga bonge moja ya mshuti kwa guu lake la kushoto lililomwacha Shaban Kado akiwa hana la kufanya uwanja wa Uhuru.
Miraj amefichua kuwa alipokuwa nje alikuwa akiusoma mchezo na kujua wapi mabeki wa Mtibwa walikuwa wamewaweza Simba.
"Nikiwa nje sikuwa na kazi ya kufanya zaidi ya kuutazama mchezo namna Mtibwa walivyokuwa wakiisumbua timu yangu, Kocha Mkuu alinipa maelekezo na kazi ya kufanya ndani ya uwanja.
"Niliambiwa ninapaswa niombe mpira mbele na sio nyuma na hicho ndicho ambacho nilikifanya mwisho wa siku tumepata ushindi ni jambo la furaha kwetu," amesema.
Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 17 huku lile la kusawazisha kwa Mtibwa Sugar likifungwa na Rifat Khamis akimalizia pasi matata ya kona iliyopigwa na Ismael Magesa dakika ya 20.
Ni mwanzo mzuri kwa Miraji Athumani, Dk chache alizopewa ktk mechi mbili kafunga magoli mawili!
ReplyDeleteWELL DONE MILAJ JR
ReplyDelete