BIGIRIMANA ATANGAZA MAUAJI AKICHEZA NA MOLINGA, MSOME HAPA
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mnyarwanda, Issa Bigirimana, amesema kuwa wiki ijayo ataanza mazoezi rasmi na timu huku akimwambia kocha wake Mkongomani, Mwinyi Zahera kuwa kama anataka tiba ya mabao, basi ampange na David Molinga ‘Falcao’.
Kocha wa timu hiyo anaifanyia kazi safu ya ushambuliaji kutokana na ubutu wa washambuliaji wake ambao wamekuwa wakishindwa kuzitumia vema nafasi za kufunga.
Bigirimana aliyepewa jina la Walcott alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu akiuguza maumivu ya paja aliyoyapata wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
Bigirimana alisema kuwa amekuwa akiumia akiona washambuliaji wenzake wakishindwa kutumia vema nafasi wanazozipata.
Bigirimana alisema atakaporejea uwanjani, angependa kupangwa kucheza pamoja na Molinga atakayecheza namba tisa na yeye kumi ili kuhakikisha wanalimaliza tatizo hilo la ufungaji.
“Molinga alikosa mechi fitinesi tu wakati anakuja Yanga, kwani alichelewa kujiunga na timu tofauti na wachezaji wengine kama mimi tuliowahi ‘pre season’.
“Nina imani kubwa na Molinga, nikuhakikishie kuwa kama nikirudi na nikipangwa kucheza naye pamoja katika safu ya ushambuliaji, basi tutafunga mabao.
“Kwangu mimi ni mshambuliaji bora mwenye uwezo wa kucheza namba tisa katika timu, ana kasi, nguvu na akili nyingi za kufunga mabao, wale wanaobeza kiwango chake nakuhakikishia atawanyamazisha hivi karibuni.”
0 COMMENTS:
Post a Comment