MLINDA
mlango namba moja wa Simba, Aish Manula amesema kuwa msimu huu Simba ina nafasi
kubwa ya kutetea ubingwa kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.
Manula msimu
uliopita aliweka rekodi mbili kimataifa kwa kuipeleka Simba hatua ya robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
hatua ya makundi ya Afcon tayari amedaka mechi mbili na Simba ilibeba pointi
zote sita.
Manula amesema kuwa nafasi ni kubwa kwa Simba kutwaa
ubingwa jambo ambalo linawafanya wapambane muda wote.
“Tunakikosi
kipana chenye wachezaji wengi na wa aina tofauti ndio maana hata kwa upande
wangu tupo magolikipa zaidi ya wawili na wote ni bora hapo ndipo changamoto
inaanzia.
“Bado nafasi
ni kubwa kwa timu yetu kutwaa ubingwa kikubwa ni sapoti kwa mashabiki na sisi
wachezaji kuongeza juhudi kwani ligi ni ngumu na kila timu inahitaji ushindi,”
amesema Manula.
0 COMMENTS:
Post a Comment