GENERATION FOOT YA SENEGAL YAGOMEA MECHI CAF VS ZAMALEK BAADA YA KUBADILISHIWA RATIBA
Imeelezwa kuwa klabu ya Generation Foot ya Senegal imegoma kucheza mchezo wa raundi ya pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek, sababu ni Zamalek kubadilisha siku ya mchezo na uwanja ndani ya saa 24.
Awali mchezo huo ulipaswa ufanyike jana kwenye uwanja wa PetroSport lakini ulisongezwa mbele hadi leo katika dimba la Borg El Arab uliopo Alexandria.
Generation Foot ambayo ilishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 tayari imeshaanza safari ya kurejea Senegal na imesema itawashitaki Zamalek na CAF kwenye mahakama ya CAS kwa kutofuata taratibu za mpira baada ya kubadili uwanja na siku ndani ya mchezo kwa saa 24 tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment