September 29, 2019


Ally Ally ni beki mzuri na sote tunakubali, lakini mara zote amecheza pembeni kama Boxer akiwa majeruhi, basi amekuwa na matatizo.

Huenda Kocha Mwinyi Zahera ANAMUAMINI lakini kuna tatizo ambalo limekuwa likiipa Yanga wakati mgumu.

Mechi dhidi ya Township Rollers, alipitika mara nyingi na tatizo lilionekana ni ule mwendo wa kuondoka haraka anapokuwa na mshambulizi.

KAWAIDA mabeki wa kati wanakuwa na kazi ha kumalizia tofauti na pembeni ambako kitaalamu wanatakkwa kucheza watu wenye spidi kwa maana ya mabeki au viungo.

Spidi ya Ally inaweza kuwa bora katikati kwa kuwa kuna m changamano wa Watu wengi. Lakini pembeni kuna TATIZO kwake na Zahera aidha alifanyie kazi au asimtumie.

Bao la Kwanza la Zesco lilifungwa na Were mbele yake. Hapa si suala la pembeni ila spidi yake yeye na kwa kuwa alikuwa dhidi ya mtu wa pembeni ALISHINDWA kumdhibiti. Angalia mechi ya kwanza Dar, Mapinduzi Balama alimdhibitj Were vilivyo na bado akashambulia.

Bao la pili, limeanzia kwake baada ya kugeuzwa pembeni ikawa kazi kwake kumuwahi wingi aliyepiga krosi DONgo na Makame akajifunga wakati akijaribu kuokoa.

Yanga wamebaki kuwa Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa katika msimu wa 2019/20. Kuna kila sababu ya kujipanga kwenye kila walochokosea katika Champions League ili kuwa imara zaidi katika Kombe la Shirikisho.

1 COMMENTS:

  1. wachambuz wa mpira tz hawajawah kuacha kukosoa, vijqna jana walijitahid kadir ya uwezo wao, ikumbukwe huyu makame ndiye litaka kulia baada ya zesco kurudisha goli dakika za mwisho.
    bi kiasi gani dogo anaifia timu, Ally Ally atalaumiwa kwa mengi lkn ikumbukwe ushiriki wake mechi za kimataifa, anamkaba nani, leo hii mtazame ubora wa yondani ukadhan anaweza mkimbiza na kumkaba mane,au salah.
    Tusipokubali kushindwa na kuzidiwa viwango kila siku tutalaumu wachezaji na kuwakatisha tamaa.
    leo Ally Ally akisoma jumbe hizi kuwa yy ndiye amesababisha mgoli matatu kufungwa ynga huyu kijana atakuwa ktk hali ganu,
    mbona mengi aliyojitahidi kuokoa hatuyaweki na kuyasifia?

    yanga amefanya kwa nafasi yake na zesco walfanya kwa nafasi yao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic