UONGOZI wa
Kagera Sugar umesema kuwa kupoteza kwao mbele ya Simba sio mwisho wa ligi
watakaza kwenye michezo yao yote iliyobaki ikiwa ni pamoja na wa leo dhidi ya
JKT Tanzania.
JKT Tanzania
inakaribishwa leo na Kagera Sugar ikiwa imetoka kushinda mbele ya Biashara
United bao 1-0 huku Kagera Sugar wao wakiwa wamejeruhiwa na Simba kwa kufungwa
mabao 3-0.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wameachana
na maumivu ya kupoteza mbele ya Simba sasa wanazitaka pointi tatu za JKT
Tanzania.
“Tumepoteza
mchezo wetu uliopita haina maana kubaki kuufikiria sasa tunahitaji kuona
tunapata matokeo mbele ya wapinzani wetu hakuna namna nyingine,” amesema.
Mohamed
Abdallah ‘Bares’ Kocha wa JKT Tanzania, amesema kuwa wamejipanga kuendeleza
furaha ya mashabiki wa JKT Tanzania watacheza kwa tahadhari kupata ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment