MTIBWA
Sugar, leo inaingia kwenye mtihani mwingine mzito ndani ya Ligi Kuu Bara kwa
kucheza na Mbeya City ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 2-2 na
Lipuli FC ya Iringa.
Mpaka sasa
kwenye michezo minne imelazimisha sare moja, imepoteza michezo mitatu na ina
pointi moja ikiwa nafasi ya 19 jambo linaloongeza presha kwenye mchezo wa leo uwanja
wa Jamhuri, Morogoro.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa
wamekuwa wakifanyia kazi makosa yao hasa kwenye safu ya ushambuliaji wana imani
ya kupata matokeo.
“Tatizo
kubwa limekuwa kwenye safu ya ushambuliaji kushindwa kumalizia nafasi ambazo
wanazipata ila kwa sasa tuna amini tutafanya vema na kupata matokeo chanya
mbele ya wapinzani wetu,” amesema.
Mtibwa Sugar
imeikaribisha mara sita Mbeya City Morogoro, imeibuka na ushindi mechi tatu na
nyingine tatu waligawana pointi tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment