KAGERE SHEVA WAINGIA KAMBANI MARA NYINGI ZAIDI
Na George Mganga
Straika wa Simba, Meddie Kagere na Miraji Athuman 'Sheva' wameongoza kuingia kambani mara nyingi ndani ya kikosi cha Simba msimu huu.
Mpaka sasa Sheva amefunga jumla ya mabao matatu huku Meddie Kagere akiingia kambani mara sita (6).
Mbali na Kagere, beki wa kushoto, Mohammed Hussein naye amefunga bao moja (1) ikiwa ni dhidi ya Kagera Sugar, katika ushindi wa mabao 3-0, bao ambalo limeifanya Simba kufikisha idadi ya mabao 10 ndani ya mechi nne ilizocheza.
Katika mechi hizo, Kagere amezifunga JKT Tanzania (mabao mawili), Kagera Sugar (mabao mawili), Mtibwa Sugar (bao moja) na Biashara United (bao moja).
Miraji Athuman amefunga bao kwa kila mechi dhidi ya JKT Tanzania, Mtibwa Sugar na Biashara United.
Katika mechi zote nne alizocheza Sheva, bao pekee alilofunga akianza katika kikosi cha kwanza ilikuwa ni dhidi ya Biashara wakati zingine zote alianzia benchi.
0 COMMENTS:
Post a Comment